Baada ya kukabidhi magari mawili na pikipiki kumi kwa wasikilizaji wake kupitia shindano la shikandinga , EFM redio inakuja na donge nono kupitia mchezo wa sakasaka ambao huchezeshwa kila mwaka toka kituo kianzishwe.
Saka saka ni shindano ambalo efm redio huficha kitu katika eneo ambalo hata hivyo msikilizaji hupewa maelekezo yake ambapo atatakiwa kwenda katika eneo hilo na kukitafuta hicho kitu kulingana na shindano.
Mwaka huu mchezo wa sakasaka utaanza tarehe 12/06/2016, utachezeshwa katika wilaya tano (5) ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Mkuranga, na Kisarawe ambapo jumla ya kiasi cha milioni tatu (3) kushindaniwa katika kila wilaya.
Ili kuweza kushiriki katika mchezo huu jamii inapaswa kusikiliza kwa makini vipindi vya redio ambapo atapata dondoo za jinsi mchezo utavyokua ukichezwa
Lengo madhubuti la mchezo huu ni kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine kwani pesa ambazo watajishindia zitawasaidia katika maisha yao kiujumla kama biashara, familia, elimu, n.k
“Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wanachangamoto nyingi za maisha hivyo kama redio tunawawezesha kwa kupitia vitu tofauti tofauti ambavyo vitawasaidia kujikwamua kimaisha”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...