Na Zuena Msuya, Bagamoyo Pwani
Wizara ya Nishati na Madini imesema itaendelea kuimarisha
miundombuni ya upatikanaji wa huduma ya umeme wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara
yanayotolewa na wateja.
Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi
Leornard Masanja alisema hayo wilayani Bagamoyo baada ya
kufanya ziara katika Ofisi ya shirika la umeme nchini (Tanesco) hivi
karibuni.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhandisi Masanja alielezwa kuwa transfoma
56 ziliibwa mafuta na kusababisha wananchi wengi kulalamikia
Tanesco kwa kuchelewa kuwapatia huduma ya umeme licha ya
kukamilisha hatua zote za kuunganishwa na huduma hiyo na umeme
kukatika mara kwa mara.
Baadhi ya transfoma zilizoibwa mafuta zikiwa katika ofisi ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Pia alielezwa kuwa, Tanesco imekuwa ikichelewa kutatua
changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo pindi
inapotokea hitilafu ya umeme au kukatika kwa huduma ya umeme
katika eneo fulani la Wilaya na Mkoa huo.
Baada ya kupokea malalamiko hayo, Mhandisi Masanja aliwataka
Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na
Meneja wa Wilaya ya Tanesco wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi
Julius Doyi kutoa ufafanizi wa namna ya kukabiliana na changamoto
hizo pamoja na kutatua malalamiko hayo kutoka kwa Meneja
Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na Meneja
wa Wilaya ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi.
Kwa upande wake Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin
Madulu, alisema kuwa malalamiko hayo yanatokana na uchache wa
miundombinu hasa kwa wale wanaohitaji kuunganishiwa huduma ya
umeme.
Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja( wa pili kulia) akikagua baadhi ya trasfoma zilizobiwa mafuta katika ofisi ya Tanesco wilayani Bagamoyo, kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu na Meneja Tanesco Wilaya ya Bagamoyo ( kushoto).
Aidha alifafanua kuwa watumishi wachache waliofukuzwa wamekuwa
wakidaiwa kuhujumu shughuli nzima za kuunganisha huduma za
umeme kwa wananchi kwa kudai rushwa kwanza jambo lililokuwa
likiwakatisha tamaa wananchi.
Hata hivyo alielezwa kuwa, tayari wafanyakazi wanane
wamefukuzwa kazi wilayani bagamoyo kwa makosa mbalimbali
ikiwemo rushwa,matumizi mabaya ya ofisi na kuchelewesha huduma
kwa wananchi.
Naye Meneja wa Tanesco wilayani Pwani Mhandisi Julias Doyi
alisema kuwa tatizo la kuchelewa kuwahudumia wananchi hasa wale
wanaopata tatizo la kukatika huduma ya umeme linatokana na
miundombinu mibovu ya kuwafikia wananchi hao na kuwa na Gari
moja la kutoa huduma kwa wilaya nzima.
Aliongeza kuwa Tanesco wamekuwa wakichelewa kupata taarifa
kutoka kwa wananchi kutokana na wengi wao kutoa taarifa hizo
kupitia Viongozi wa Serikali za mitaa na kusababisha taarifa hizo
kuchelewa kuwafikia Tanesco.
Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi
Leornard Masanja( mbele) akiwa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Martin Madulu( nyuma kulia) na Meneja wa Tanesco
Wilaya ya Bagamoyo( nyuma kushoto) wakitoka katika ofisi ya
serikali ya mtaa kupata maoni ya viongozi wa mtaa juu ya huduma ya
umeme wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...