Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa mujibu wa Kanuni ya 118 ya Kanuni za Kudumu za Bunge,  Toleo la mwaka 2016, Nyongeza ya Nane, Sehemu ya Tatu  Kifungu cha 9, imepewa jukumu la kusikiliza maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha kila mwaka. 

Katika kutekeleza jukumu hilo, Kamati ya Bajeti imepanga kufanya Mkutano wa Wadau wote wa masuala ya kodi (Public Hearing) kwa ajili ya kusikiliza maoni yao na mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016. 

Mkutano huo umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Tarehe 16 Juni 2016 kuanzia Saa Tano asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Mkoani Dodoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo: 
 
Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, S.L.P 941, DODOMA Barua pepe: cna@bunge.go.tz 
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano. Ofisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...