Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho kitaweza kufanya kazi.
"Kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,
Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume)
"Unaweza kukuta kuwa mlipa kodi kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia lakini chombo hicho kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu sahihi kama linavyotakiwa kuwapo," alisema Msangi.
Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa chombo hicho kama kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na TRA ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa kodi na wakusanyaji wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo hilo linawahusu wote.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...