Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa tawi la hospitali hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho leo kwenye ukumbi wa CPL, Muhimbili.
Wajumbe wa TUGHE wakiimba nyimbo za mshikamano leo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya.
Mmoja wa wajumbe wa TUGHE, Helmut Ngalawa akipiga kura leo kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.
Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya wajumbe kupiga kura leo kwenye ukumbi wa CPL-Muhimbili.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa TUGHE katika Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege (kulia) na katibu wake, Faustine Kaitaba wakipongezana leo baada ya kuchaguliwa tena katika nafasi hizo kuongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano.
Picha na JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...