Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi
wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Saalam. Katika kikao hicho NIDA iliwasilisha
mpango usajili kufikia 31 Desemba 2016 ambapo usajili utakamilika nchini nzima na
wananchi kuanza kutumia namba ya utambulisho kupata huduma. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed
Khamis, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho Ndugu
Alphonce Malibiche
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed
Khamis, akifafanua namna mwananchi anaweza kutumia tovuti salama kujua taarifa
zake wakati wa kikao na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa idara ya Habari
Maelezo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Hifadhi Hati wa NIDA Bi Rose Mdami.
Serikali imekusudia kukamilisha Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi
wote kufikia Desemba 31 mwaka huu.
Akuzungumza na vyombo vya habari leo, msemaji wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa Bi. Rose Mdami, amesema NIDA imepanga kutumia taarifa za
NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya Utambulisho kwa wananchi
wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA.
Akifafanua, Bi Rose amesema baada ya kuhakikisha kila mwananchi ana
Nambari ya Utambulisho, kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa
ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya
vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili.
“kama mnavyofahamu, katika usajili wa NEC fomu ilikuwa na vipengele 32
vya kujaza kulinganisha na fomu ya NIDA ambayo ina vipengele 74, hivyo ni lazima
kila mwananchi kutambua, ili kuwa na utambulisho kamili lazima kujaza vipengele
vilivyobaki pamoja na kuambatanisha nakala ya viambata vyake muhimu kuthibitisha
taarifa za umri, uraia na makazi” alisisitiza.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...