Geofrey Chambua-Mtafiti na Mchambuzi ​

Vyombo Mbalimbali vya Habari vya Ndani na Vile vya Kimagharibi Ikiwemo BBC Swahili, Jana 28/6/2016 vilitaarifu kugunduliwa kwa  gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania ambapo Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Huenda tu tujuzane ukweli kwamba Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali lukuki kiasi kwamba wengi wanashangaa kiwango kikubwa cha umasikini wa watu wake.....wacha nikujuze kidogo RASILIMALI ZA TANZANIA

1. Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 kuelekea 55 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki. Uhuru pekee ni rasilimali tosha

2 Tz ni nchi ambayo imekuwa ina kitu cha pekee ambacho nchi za Africa zimekikosa nacho ni AMANI na UVUMILIVU kwa miaka yote 54 ya uhuru 

3. Tz ina ukubwa wa 945,087 km mraba yaani sawa na uchukue Denmark, France, United kingdom (UK), Netherlands, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja. Uingereza ni ndogo mara 7 lakini ilikua ndiyo mtawala wa mwisho Tanzania. Katika ya eneo lote hilo, 30% ya Tz ni Mbuga za Wanyama. kuna Maeneo 12 ya Hifadhi Asilia, Mapori Tengefu 38. Hekari milioni 33 za misitu ambapo kuna mti wa mpingo ulio ghali zaidi duniani huku nchi ikiwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya misitu ikiwemo mbao na asali

4. Tanzania ina jumla ya watu milioni 44.9 ambapo wanawake ni 51.3 na wanaume ni 48.7%, nguvu kazi ya Taifa ni 52.2% ilihali vijana ni 66.4% (sensa 2012) hata hivyo wastani pato la kila mtu ni ni shilingi 2880 kwa siku tu huku mtu mmoja akitegemewa na wastani wa watu 8!!! asilimia 75 ya wakulima wanaingiza pato la asilimia 24 tu kwenye bajeti ya Taifa huku makusanyo ya kodi yakiwa ni shilingi trilioni 12 tu kwa mwaka katika bajeti nzima ya trilioni 23 (THDR 2014)


5. Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa kilomita 1,424; bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, gesi, utalii na nyinginezo. Mwambao wa Tanzania Una Bandari Kuu Tatu ambazo ni Mtwara, Tanga na DSM

5. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi. Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani(la kwanza afrika) na ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu afrika).

6. Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera,mto Ruvuma, mto Rufiji, mto wami, mto Malagarasi,mto mara, mto Pangani, mto mara, mto gombe, mto mweupe wa Nile. Na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbwemkuru n.k
7. Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo kwenye top 20 Duniani. Tanzania inaongoza kwa gesi Afrika ikiwa na futi za ujazo trilioni 57.27. Gesi ya Mto Ruvu Pekee iliyogunduliwa hivi karibuni ina ujazo wa futi triliobi 2.17 TU, na thamani yake ni dola bilioni sita sawa na trilioni 12 za Tz..

8. Tanzania Ina Jumla ya Migodi HAI Mikubwa 9 Kati ya Hiyo 6 ni ya Dhahabu, 1 wa Almasi upo Mwadui 1 ni wa Makaa ya Mawe Kiwira na mwingine ni wa Vito ama Tanzanite hapo Mererani

9. Hata Hivyo Tanzania ni Moja ya Nchi MASIKINI SANA DUNIANI AMBAPO ASILIMIA 30 YA WATANZANIA WANAISHI KWENYE UMASIKINI WA KUPINDUKIA (hawana uhakika mchana huu watakula nini_) tukitegemea misaada ya wafadhili na wahisani

10. CHA KUSIKITISHA ZAIDI zaidi ni ni kwamba Tanzania ni nchi ya 159 kati ya nchi 187 Duniani kwa umasikini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2016

    Tuliposikia habari hii ya kugundulika kwa hii gesi nyepesi ya Helium wengi wetu tulikubaliana na mwandishi hapa kuwa nchi hii imebarikiwa na raslimali nyingi sana kazi kwetu kuzitumia vizuri. Balozi mmoja wa Ujerumani aliwahi kusema kabla ya kuondoka Tanzania siku za nyuma kwamba jinsi nchi yetu ilivyokuwa na raslimali nyingi kama mito, maziwa, ardhi yenye rutuba, madini, vivutio vya utalii, bandari n.k. haelewi kwa nini nchi hii ni maskini. Hii hotuba yake ilizungushwa kwenye mitandao wazawa wengi tukaijadili na wengi wetu tukakubaliana naye na kuhamasika kwamba umasikini uliopo hasa vijijini usingekuwepo kama tungekuwa tumejipanga vizuri. Wajibu wa kuondoa umasikini ni wa kila mtanzania, kila anayeweza awekeze, tabia zetu zisizoleta maendeleo na kuchangia biashara kama siwezi kula ovyo barabarani au nje ya nyumba yangu zibadilike tujenge biashara, kilimo, pesa izunguke, ili kuondoa umasikini uliokithiri katika sehemu mbalimbali. Ugunduzi wa raslimali hizi na mapato yatokanayo na nyingine zote zilenge kuinua maisha ya kila mtanzania. Viongozi wetu wanahitaji kujenga uwezo wa kuelewa mambo ya jinsi ya kuikwamua nchi hii kutokana na maisha duni ikiwemo kwenye maeneo yenye raslimali hizi. Tukidhamiria kwa dhati kabisa inawezekana kuondoa umasikini hakuna atakayetusaidia ni sisi wenyewe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2016

    Tunahitaji kubadilisha mindset viongozi wenye elimu na upeo tunao wapo wanaohitaji exposure ili waweze kujifunza kutoka nchi nyingine na kuboresha hapa nyumbani. Wananchi nao wajengewe uwezo wa kuelewa ili wasiwe kikwazo katika mabadiliko ya uchumi yatakayokuja.

    ReplyDelete
  3. SABABU WANAOONGOZA NI WEZI NA WABINAFS NA SERIKALI HAITENDI HAKI KWA RAIA ZAKE KWA UBAGUZI WA KIDINI NA MOLA HAWAPENDI MAFISADI NA WAHARIBIFU NA WABAGUZI ,,,,BILA KUREKEBISHA HAYO MAISHA YATAKUA HAYO HAYO MPAKA KIAMA ....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2016

    SASA NI TATIZO NI KUKOSA AKILI AU MAALIFA? MI NAONA NI KUKOSA MAALIFA NA UVIVU, UVIVU WA KUFIKIRI NA KUJITUMA KUFANYA KAZI KWA BIDII.HIZO NCHI ZOTE ULIZOZITAJA HAPO WALA HAWANA HUU UTAJILI WA ASILI TULIOKUWA NAO. LAKINI WAMETUZIDI NA NDIO HAO TUNAKOPELEKA VIBAKULI VYETU VYA SAIDIA BABA YAANI HATUNA HATAA AIBU SISI WAFRICA WATU WEUSI NDIO MAANA WATAENDELEA KUTUDHALAU NA HII SAIDIA BABAA

    ReplyDelete
  5. Ndugu Mtafiti na Mchambuzi,
    Makala yako ni hali halisi iliyopo na si utafiti, na kila Mtanzania anajua na wote ndio wimbo wetu ikiwemo mimi.
    Swali ni kwamba, je mimi na wewe kama watanzania, mbona hatutoi majibu? Tunalaumu na kukosoa tu. Je tunamlaumu na kumkosoa nani? Je nani aje kutubadilishia hali hiyo iwe kama ya wenzetu?

    Tufikirie majibu na siyo kuuliza au kulaumu maswala ambayo ni majukumu yetu.

    Tafakari na chukua hatua.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2016

    Wakati huu wa jitihada za kuondoa rushwa, ufisadi, ulaji, uchu wa mali ya umma, na kurudisha maadili na utii wa sheria na taratibu serikalini ni muafaka katika kuchukua hatua za kuinua maisha ya watanzania katika kona zote. Tujenge mazingira mazuri ya kuleta maendeleo endelevu ya walengwa hasa walioko vijijini. Viongozi wa ngazi zote wanatakiwa kuwa na maono na malengo yanayohusu sehemu zao ili kuiondoa nchi hii kwenye lindi la umasikini pale ulipokithiri. Viongozi kama alivyosema Cameron wa Uingereza ndio manahodha wenye dira ya kujua tunaelekea wapi katika hili la kuondoa umaskini, kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2016

    The mdudu, nyie hapo juu wote ni Shieeeda sioni mnacho lalama mimi nahisi nyie ndio mnao mpinga JPM rais mwenye zamira za ukweli na mwenye hasira na umasikini wa watanzania lakini cha kushangaza watu washaanza kumuita eti Dikiteta sasa udicteta wake ni nini wakati ana wanyoosha wale wote waliokua wanaitafuna nchi kama Mchwa sasa ndugu yangu ulie andika hii Makara umechemsha vibaya sana huu sio wakati wake ila kama ungeandika kwenye serikali zilizopita kweli ningekuona wewe ni muona mbali, sasa ushauri wangu kwako ni bora ufanye juu chini uombe kuonana na Mr President MAGUFULI coz huyu rais anawahitaji sana watu wenye mawazo mazuri kwa nchi yao ili mkae na kumpa ushauri au mikakati yako lakini sio kuandika hapa coz sisi wengine tushachoka coz rais wetu na viongozi wote kwa ujumla sio lahisi kuziona Makara kama hizi hapa kwenye Blogs kama kilio chetu kilikua hakina msikivu sasa huyu hapa leo mungu katuletea tuacheni mambo ya uvyama tuwe pamoja kwenye kuijenga Tanzania yetu. na sisi wananchi tuwe tunajiuliza nimeifanyia nini? Tanzania yangu na wala sio kulalamika tuuuu kwa Message's huku ndio kwanza uko kitandani au Bar unapiga urabu then unataka maendeleo? mjomba Michuzi please nifikishie huu UPUPU ili uwawashe vyema

    ReplyDelete
  8. Kila mnapogundua madini au gesi mfano dhahabu,almasi na kuendelea mnasema tutafute wazungu/wawekezaji waje wawachimbie na wakaiuze. Mnafikiri hao wazungu watakaotoka huko kwao waje wawachimbie madini yenu kwenye nchi yenu watamtajirisha nani kwanza/zaidi. Amkeni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2016

    Maghufuli kama atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watanzania basi ni muarubaini tosha wa umasikini Tanzania. Ni bora hao wanaomwita Maghufuli dikteta wafanye hivyo kuliko kumwita lege lege. Kutokana na hulka ya ulegevu wa akili na vitendo kwa watanzania katika kujitafutia maendeleo lazima apatikane kiongozi dikteta tena wa ukweli kabisa. Wanaosema Magufuli dikteta ni hao kati ya watanzania wenye akili lege lege na hapana shaka wanahitaji kunyooshwa ili akili zao zikazane kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...