Mkurugenzi Mkuu  Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA), Dk.Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali wakati wa kuwakabidhi vyeti vya ushiriki wa mkutano huo uliofikia tamati ukumbi wa Veta mjini Morogoro leo jioni.
Mkurugenzi Mkuu  Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA), Dk.Allan Kijazi (kulia), akiwa na viongozi wengine kabla ya kuanza zoezi la kutoa vyeti kwa wanahabari washiriki wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Jaji Tuzo za Habari za Tanapa, Jack Muna, Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori), Dk.Felician Kalahama na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko, Ibrahim Mussa.
Mkurugenzi Mkuu  Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA), Dk.Allan Kijazi (kulia), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Mhariri wa gazeti la Jambo Leo, Joseph Kulangwa.
Mpiga picha Loveness Benard wa gazeti la Tanzania 
Daima akikabidhiwa cheti. Nyuma yake ni Mpiga picha wa Daily News/Habari leo na Blogger Mroki Mroki "Father Kidevu".
Wanahabari wakimsiliza Dk. Kijazi wakati akifunga mkutano huo. Wa pili mstari wa katikati ni  Nelly Mtema wa Daily News akifuatiwa na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii aliyeiwakilisha Michuzi Media Group.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...