Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa
kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous
na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati
alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la
Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa
na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip
way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika kama nyenzo muhimu katika
kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia
baadhi ya picha katika kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika
Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na
Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto) wakati alipomtembelea
leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha
picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa
kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho kitakuwa ni
nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za
Kimataifa.
Huu ni mwonekano wa nje wa kitabu cha Picha zilizochukuliwa katika
Pori la Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert
Ross, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof.
Maghembe ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina
Madete katika hoteli ya Slipway.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...