Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja
Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani
kulipa posho ya chakula kwa watu ambao
si askari.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank
Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya
malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000 kama
posho ya chakula kwa watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Meja Jenerali Rwegasira
amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani
‘ration allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.
Meja Jenerali Rwegasira amesema
anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha
uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma zinazomkabili.
Katibu Mkuu huyo amesema
baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi
wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili
kufanikisha malipo hayo hewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...