Uongozi wa Kampuni ya Business Times Limited (BTL), inayozalisha Magazeti ya Business Times, Majira na Spoti Starehe, inasikitika  kutangaza kifo cha mfanyakazi wake Elizabeth Mayemba (pichani).

Elizabeth Mayemba ambaye alikuwa ni Kaimu Mhariri wa Michezo Gazeti la Majira alikutwa na mauti Jumamosi ya Julai 9, 2016 saa 2 usiku, akiwa nyumbani kwake Tabata Kisukulu, Dar es Salaam.
Kabla ya kukutwa na mauti, marehemu alifanya kazi zake na majukumu yote ya kila siku bila kuonesha dalili za kuumwa.
Akiwa nyumbani kwake saa 2 usiku, alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Amana, akiwa njiani alikutwa na mauti.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Elizabeth Mayemba atazikwa siku ya Jumanne ya Julai 12, 2016, mkoani Morogoro kwenye Makaburi ya Kola.
Elizabeth Mayemba ataagwa Jumatatu ya Julai 11, 2016 saa 5.00 asubuhi nyumbani kwake Tabata Kisukulu. Baada ya Misa mwili utasifirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kila mara ili kuwapa nafasi watu wengi wajue ratiba zote zilivyopangwa.
Kampuni imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Elizabeth Mayemba, ambaye mchango wake ulikuwa mkubwa zaidi na ulioonekana kwa kila mtu. Marehemu ameacha mume na watoto watatu wa kiume.
Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. 
Amina

Meneja Mkuu
Business Times Limited

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duu...uongoz unapenda kutangaza kifo? I thought unasikitika...kumbe unapenda!
    Muwe mnahakiki munayoandka kabla ya kupost

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...