Kampuni
ya ORIFLAME imezindua bidhaa zake mpya kwenye soko la Afrika Mashariki
ambapo vipodozi maalum vitakavyokufanya ngozi yako kuonekana yenye
kukaa na safi wakati wote kwa ngozi imeingia dukani kwa sasa.
Bidhaa hiyo maalum ni ya kusaidia ngozi kung’aa ambapo watumiaji wa bidhaa za ngozi wameshahuriwa kutumia bidhaa hiyo kwani imetengenezwa kwa vitu halisi ikiwemo matunda,mimea na majani ya hasili na kufanya ngozi kuwa katika hali ya afya wakati wote wa matumizi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bi. Mary Riung amebainisha kuwa, bidhaa hizo zitasaidia watu wengi kwani zimetengenezwa kwa ubora.
“Bidhaa hizi ni nzuri kwani zitakufanya kuweka ngozi yako kuwa nzuri ikiwemo kuondoa makunyanzi, kuondoa madoa na kufanya kuwa na rangi moja usoni. Ni bidhaa bora na itapatikana kwetu pekee katika soko la hapa Tanzania na Afrika Mashariki” alieleza Mary Riung.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Piyush Chandra amebainisha kuwa, kampuni hiyo ambayo ilianzishwa tokea 1967 imekuwa ni miongoni mwa makampuni yanayofanya vizuri katika bidhaa zake na watu wengi wametokea kuipenda hivyo kwa bidhaa zao zote wanazotengeneza zimeendelea kuwa na ubora Duniani kote.
Miongoni mwa bidhaa zao ni pamoja na NovAge ambayo imetengenezwa mahususi kumfanya mtumiaji ambaye ngozi yake imeonekana kuzeeka na endapo ataitumia vipodozi hivyo vitamfanya kumuondolea hali hiyo na kuonekana safi kama kijana kwani inaondoa makunyanzi ndani ya kuanzia wiki 12 huku ikiwa imethibitishwa na wataalamu kwa kuongeza ‘collagen kwa asilimia 200.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...