Na Bashir Yakub.

Marejeo ya makala haya ni katika makosa ya madai yaliyo katika mashauri ya madai. Japo jambo hili lipo hata katika makosa ya jinai yumkini makala hayatajielekeza huko.

Basi yafaa ifahamike kuwa mtu aliyeshitakkiwa kwa kosa fulani, kesi ikasikilizwa na hukumu ikatolewa akashinda au akashindwa, ni kuwa kesi ya namna hiyo haitakiwi kufunguliwa tena. Isifunguliwe tena katika mahakama hiyohiyo au mahakama nyingineyo nchini.

Haiwezekani kesi iliyosikilizwa na kutolewa maamuzi kufunguliwa tena. Yapo mambo yanayoweza kufuata baada ya kesi kuisha kwa mfano rufaa, marejeo, na mapitio lakini sio kufungua tena upya.

1.MAMBO YANAYOZINGATIWA.

Yapo mambo ya kuzingatia ili kesi iliyokwisha isifunguliwe tena. Kwanza ni lazima wahusika wawe ni walewale. Haiwezekani Shaaban alimfungulia kesi Maria ikasikilizwa na kutolewa maamuzi halafu shaaban huyohuyo akamfungulia tena Maria kesi ileile kwa kosa lilelile.

Shaaban anaweza kumfungulia Maria kesi nyingine ikiwa ni kwa kosa tofauti na lile la awali lililokwisha kuamuliwa . Utaona hapa kuwa kinachozuiwa ni mtu yuleyule kumfungulia mtu yuleyule kwa kosa lilelile.

2. NINI UFANYE HILO LIKITOKEA.

Iwapo hili litatokea wenye wajibu wa kulizuia ni watu wawili. Kwanza ni wajibu wa mshitakiwa kuieleza mahakama kuwa kesi hii ilishahukumiwa sehemu fulani na hapa imerudiwa. Ni wajibu kwa mshitakiwa au mwakilishi wake awe wakili au vinginevyo.

Pili ni wajibu kwa jaji anayesikiliza au hakimu anayesikiliza kesi hiyo kufanya utafiti kupitia kumbukumbu za mahakanma na kuliona hilo ili kulizuia. Hata hivyo wajibu mkubwa ni mshitakiwa kwakuwa jaji au hakimu wakati mwingine anaweza asiligundue hilo hasa ikiwa kesi hiyo iliisha mahakama nyingine na sasa imefunguliwa upya mahakama nyingine.

Hivyo tunaweza kusisitiza kuwa wajibu mkubwa upo kwa mshitakiwa mwenyewe kwasababu yuko katika nafasi nzuri ya kujua historia ya kesi yake kuliko mwingine awaye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...