Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mohammed Mtanda amekabidhiwa rasmi ofisi ya Wilaya hiyo na mtangulizi wake, Idd Hassan Kimanta ambaye amehamishiwa Wilaya ya Monduli.
Akizungumza katika makabidhiano hayo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kumpa Mkuu wa sasa wa Wilaya hiyo, Saidi Mtanda ushirikiano na kuendeleza undugu na uchapakazi.
“Ndugu watumishi wenzangu, mimi naondoka ila sina wasiwasi na Mkuu wa Wilaya mpya kwakua namfahamu tangu akiwa mwalimu kule Bagamoyo, mpeni ushirikiano, ni msomi mzuri na mchapa kazi” Alisema Kimanta.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda alimshukuru Kimanta na kuahidi kuyaendeleza yale yote mema aliyoyaacha.
“Ndugu zanguni, kila zama na kitabu chake, Kimanta ametimiza wajibu wake na sasa amehamishwa kituo kingine cha kazi ili kuendeleza gurudumu analo niachia la kumsaidia Rais kuwahudumia wananchi, Mimi si mtu wa kukaa ofisini, ni vyema mkajiandaa kisaikolojia kwa kauli mbiu ya kuwahudumia wananchi ambayo huwa naisema mara kwa mara kwambaa jukumu letu ni Kuwapokea Wananchi, Kuwasikiliza na Kuwahudumia” Alisema Mtanda
Mara baada ya makabidhiano hayo, Mtanda akakutana na makundi mbali mbali ya vijana wajasiriamali ambapo alisisitiza juu ya azma ya uongozi wake wilayani humo wa kuwaajengea mazingira wezeshi makundi mbali mbali ili yaweze kujiajiri hivyo kupunguza utegemezi na umasikini.
Katika hali ambayo wakazi wengi wa wilaya hiyo hawakutarajia, Mkuu huyo wa Wilaya akawakusanya madereva pikipiki marufu kama boda boda huku akiambatana na Kaimu Kamanda wa Polisi wa wilaya na akawataka wamueleze changamoto wanazo kutana nazo kisha akatoa maagizo kwa Kaimu Kamanda wa Polisi wilayani humo kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya madereva wa pikipiki wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...