Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
MISS Dar Indian Ocean 2016 wamekabidhiwa gari na kampuni ya Helmic Group Company Limted ikiwa ni maandalizi kuelekea shindano hilo linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni linaloandaliwa na Succesfull Fashion Desginer .

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa gari hilo aina ya Coaster litakalokuwa linatumika kwa ajili ya kuwapeleka warembo hao sehemu mbalimbali, Msemaji na mratibu wa warembo hao Sarah Martin ameshukuru kwa hatua hiyo kutoka Helmic  na kusema kuwa hiyo ni hatua nzuri kwao kwani kwa warembo waliokuwa wana uhakika wa kulibakiza taji la Miss Tanzania kutoka Miss Dar Indian Ocean. "Kutoka Miss Dar Indian Ocean tumeweza kutoa warembo mbalimbali na waliweza kuwa Miss Tanzania na hilo tunajivunia sana kwani ukiangalia Nancy Sumari, Wema Sepetu, Richa Adhia na Faraja Kota wote wametoka hapa,".

Amesema kuwa, moja ya malengo yao makubwa  ni kuweza kuwasaidia warembo hawa kufika mbali hususani kwenye masuala ya urembo ukizingatia tuna kampuni inayojihusisha na mitindo basi hatutaweza kuona wanaishia na kupotea zaidi tutawachukua na kufanya nao kazi zaidi ya hapa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampini ya Helmic Group Harprit Kaur Sohal amesema kuwa huu ni mwanzo ila malengo yao makubwa ni kuwasaidia warembo hawa katika shindano lao Miss Dar Indian Ocean na zaidi wamewapatia gari hilo kwa ajili ya kuwarahisishia kwenye shindano lao na amewataka warembo kujiamini zaidi.

Mshiriki wa Dar Indian Ocean, Neema Steven Dismas amesema kuwa akifanikiwa kushinda taji hilo ana imani atazidi kuiwakilisha nchi yetu vizuri hasa akiweza kwenda kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutumia nembo ya Taifa ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama na lugha adhimu ya Kiswahili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Heelmic Group, Harprit Kaur Sohal akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akiwakabidhi Miss Dar Indian Ocean gari leo Jijini Dar es Salaam.
 Msemaji na Mratibu wa Miss Dar Indian Ocean, Sarah Martini akizungumza na kutoa shukrani wakati wa kukabidhiwa gari na mkurugenzi Mtendaji wa Helmic Group Harprit Koul Sohal (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam, shindano hilo linatarajiwa kufanyika mapema hivi karibuni.
Warembo wa Miss Dar Indian Ocean wakiwa mbele ya gari aina ya Coaster waliopatiwa kwa ajili ya matumizi wakati wakiwa kambini ambapo mashindano hayo yatafanyika hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...