Hatimaye mwenge wa Uhuru umewasili Wilayani Nkasi huku sherehe hizo zikishereheshwa na mihemko ya wakazi wa maeneo mbalimbali wilayani humo wakiwa na shauku ya kujua ni miradi ipi itazinduliwa ndani ya jamii zao ambayo huenda miradi hiyo ikawa muarobaini wa matatizo chungu mzima yanayo wakabili.

Shauku ya wakazi wa Wilaya hiyo inaondolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Said M.Mtanda ambapo akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo katika risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ana ainisha kwamba mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zimepitia miradi 11 yenye thamani ya Tsh.7,056 (Bil) huku vipaumbele vikiwaa ni uwezeshwaji wa vijana na wanawake pamoja na makundi maalum huku elimu ikipewa kipaumbele.
Mkuu wa Wilaya Sumbawanga Dr.Halfan Boniface Haule (Kushoto) Akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh.Said Mohamed Mtanda
Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa kwa shule mbalimbali Wilayani Nkasi wakati wa Sherehe za mbio za Mwenge wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...