Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi.

Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).

Akizungumza na Mtandao huu, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.

Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi na viwango vya Kimataifa.

Wakati huohuo, TFF inatarajia kuimarisha Kurugenzi yake ya masoko ambako sasa ataajiriwa Mkurugenzi wa masoko na habari.

Lengo has ni kuendana na halihalisi ya uendeshaji mpira duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.

Lengo ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpirwa a miguu zinatokana na mpira wa miguu na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati muafaka “ Alisema Mwesigwa Selestine”

Kwa nafasi za kazi katika TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...