Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika katika mji wa Sao Paulo, Rio De Jeneiro nchini Brazil , timu ya kuogelea imefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya kukabidhiwa bendera na Kamati ya Olimpiki nchini TOC kwa ajili ya kuiwakilisha vyema katika mashindano hayo.

Timu hiyo itakayowakilishwa na waogeleaji wawili ambao ni Magdalena Moshi anayeenda kwa mara ya tatu kwa upande wa wanawake huku Hilal Hilal akienda kwa mara ya kwanza na wote watakuwa ni waogeleaji katika upande wa mita 50. Akizungumzia maandalizi ya mwisho Kocha wa timu hiyo Alexandra Mwaipasi amesema kuwa wachezaji wake wameiva kwani mwanzoni walikuwa na changamoto ya kupata mabwawa yenye viwango vinavyoendana na mashindano hayo ila kwa mwaka huu washiriki wote wameweza kuweka kambi katika nchi mbili tofauti ambapo Magdalena amekuwa Australia huku Hilal akijifua nchini Dubai.

Amesema, ana imani na wachezaji wake kwani kwa kipindi alichokaa nao ameona uwezo waliokuwa nao na  wanaweza kurudi na medal nyumbani. Naye Katibu mkuu wa chama cha kuogelea TSA Ramadhan Namkoveka amesema kuwa tofauti na wengine wao hawajapata wadhamini ila wachezaji wao wamejiandaa vizuri na wana imani kubwa kuwa wataweka historia.

Moja ya washiriki, Magdalena Mosha amesema kuwa amejiandaa vizuri na anaamini miaka aliyoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing na London yamempa uelewa zaidi wa nini anatakiwa kufanya mwaka huu na katika mazoezi yake nchini Australia  ameyafanyia kazi. Amesema kuwa kwa sasa macho ya watanzania yapo kwao na wanatoa ahadi ya kufanya vizuri kwani hata mshiriki mwenzie  Hilal amekuwa kwenye mazoezi mazuri nchini Dubai tena katika kituo kinachojihusisha na masuala ya uogeleaji.

Timu hiyo kesho inakabidhiwa bendera na TOC kabla ya Agosti 02 kuondoka kuelekea nchini Brazili.
Magdalena na Hilal wakiwa katika mazoezi ya mwisho.
Magdalena Mosha akiwa pamoja na mshiriki mwenzie Hilal Hilal wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya kuondoka kuelekea nchini Brazil.
Viongozi wa Chama cha Kuogelea TSA wakiwa pamoja na washiriki Hilal Hilal na Magdalena Mosha, Kushoto ni mkurugenzi wa ufundi Amina Mfaume, Mwenyekiti wa TSA Alex Mosha, Katikati ni Kocha wa timu ya kuogelea Alexandra Mwaipasi na mwisho kulia ni Katibu mkuu TSA Ramadhan Namkoveka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani hii swimming pool mbona kama ya nyumbani? Olympics size swimming pool ndio inatakiwa wafanyie mazoezi.

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa nafikiri chama cha kuogelea kinalia kila siku kwa serikali yao kuwa na bwawa la kimataifa lenye viwango vilivyothibitishwa na FINA. Kwa mawazo yangu hili ndilo bwawa lililopo hapa Tanzania kwa ajili ya waogeleaji wetu wafanyie mazoezi.

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa mpaka sasa Tanzania hakuna swi mmimng pool yenye hadhi ya kimataifa. Ni vizuri serikali ikatekeleza wazo la Mheshimiwa Benjamini Mkapa wa kujenga pool pale uwanja wa Taifa. Kwa hakika hii itasaidia kuwa na watu wengi wanaojishughulisha na kuogelea na hatimae kuwa na wachezaji wenye viwango.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...