Ilikuwa ni fainali mbovu kumalizia michuano mikali ya Euro 2016. Yaani Ureno, ambayo imenyakua ubingwa huo kwa goli moja la mshambuliaji wa zamani wa Swansea ya Uingereza Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes, timu iliyomaliza ya tatu kwenye hatua za makundi wamenyakua kombe wakiwa wameshinda mchezommoja tu kati ya saba ndani ya dakika 90. Hata hivyo Ureno inastahili sifa, kwanipamoja na kumpoteza nahodha wao na mchezaji Bora Cristiano Ronaldo alipoumia goti katika kipindi cha kwanza kwa kuchezewa vibaya na Dimitri Payet wa West Ham.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ureno wakishangia kwa pamoja ushindi walioupata kupitia kwa Mshambuliaji, Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes (9) wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji wa Mashindano hayo, Ufaransa, uliochekwa katika uwanja wa Stade de France.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Christiano Ronald pamoja na Mkongwe Ricardo Quaresma wakiwa na mwali wao mara baada ya kutwaa kwa kuwagaragaza wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) katika mchezo uliopigwa katika dimba la Stade de France, nchini Ufaransa.
Huzuni baada ya kufungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...