·
Tamasha
hilo litafanyika siku ya Jumamosi, Agosti 13, 2016 katika viwanja vya posta
Kijitonyama.
·
Wasanii
wakubwa nchini kulishambulia jukwaa, wakiwemo Ali Kiba, Lady Jaydee, Yamoto
Band, Madee, Juma Nature, Snura, Stamina, Eskide (msanii wa muziki wa singeli)
na bila ya kusahau wakali wa bongo movie pia watakuwepo.
·
Watanzania
wataweza kujionea jukwaani vipindi mbalimbali vinavyorushwa kupitia chaneli
hiyo inayoonekana hapa nchini Tanzania na Kenya.
Wasanii wa muziki wa Bongo Flava
Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la kusherehekea
miaka miwili tangu kuanzishwa kwa chaneli ya StarTimes Kiswahili siku ya
Jumamosi ya Agosti 13, 2016 katika viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes
Tanzania, Bw. Damien Li amesema kuwa tamasha hilo linadhamiria kusherehekea kwa
pamoja na wateja wao mafanikio yaliyofikiwa na chaneli ya StarTimes Kiswahili
katika kuonyesha vipindi vyenye maudhui ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya.
“Chaneli hii mwaka huu mwezi wa
Agosti inatimiza miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mnamo Agosti mosi mwaka
2014. Chaneli ya StarTimes Kiswahili inaonekana katika nchi mbili za Tanzania
na Kenya na hivyo kutoa wigo mpana kwa wasanii na watayarishaji wa vipindi hapa
nchini kupata fursa ya kuonekana maeneo hayo. Vipindi vingi katika chaneli hii
huangazia masuala ya filamu, muziki, burudani, vyakula, mitindo ya maisha na
mavazi pamoja na tamaduni za watu wa Afrika ya Mashariki hususani kwa nchi hizo
mbili ambavyo huwasilishwa kwa lugha ya Kiswahili.” Alisema Bw. Li
“Tamasha hili litahusisha shughuli
mbalimbali hususani kuangazia maudhui yanayopatikana kwenye chaneli ya
StarTimes Kiswahili lakini pia litapambwa na burudani kadhaa kutoka kwa wasanii
watakaoalikwa. Siku hiyo watanzania watawashuhudia wasanii wakubwa wa muziki wa
bongo flava jukwaani kama vile Ali Kiba, Lady Jaydee, Juma Nature, Madee, Yamoto
Band, Snura na Stamina.

Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza kwa makini kulia ni Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li na kushoto ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la StarTimes Kiswahili linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL, Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li, Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba na Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian wakikata keki kuashiria uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Waandaaji,Wadhamini na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye tamasha la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL wakiwa katika picha ya pamoja.
Mmoja wa Wasanii atakaetumbuiza kwenye tamasha la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL Ali Kiba akipeana mkono na Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian.
Baraza la Kiswahili jitahidini kutoka na kukemea watu wanao potosha Kiswahili hasa kwenye matangazo ya kitaifa na kimataifa, mfano hilo neno "SEREBUKA" HILI SIO NENO LA KISWAHILI na kama walitaka kusema SELEBUKA basi lingeandikwa kifasaha kama walivyoweza kumalizia sentensi nzima kwa maneno ya kingereza kwa ufasaha, tukiachia haya yaendelee bila kuwa na mlinzi wa kuitunza lugha hii basi itafika pabaya, siku hizi unaona hata magazeti yanashindwa kuandika Kiswahili fasaha hii ni aibu kwenu nyie baraza la Kiswahili kwa kukaa kimya bila kukemea hii tabia.
ReplyDelete