Waombolezaji
wakilishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa
mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wa mazishi yake
yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu
wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Marehemu Senga alifariki wiki iliyopita
nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo. Mungu ailaze roho
yake mahala pema peponi AMIN.
Mjane
wa Marehemu Joseph Senga, Bi. Winfrida Senga akiweka shada la maua
kwenye Kaburi la Mumewe, wakati wa mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo
kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti hili, marehemu Joseph Senga wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.

Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa akiweka shada la Maua.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ambaye
pia ni Mmiliki wa Kampuni ya FreeMedia wachapishaji wa Gazeti la
Tanzania Daima alikokuwa akifanya Kazi Marehemu Joseph Senga, akitoa
salamu za Rambirambi, wakati wa Mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo
kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.
Ibada ya Mazishi ikiendelea.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiweka shada la maua kaburini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...