Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakiwa wameshika Hati za makubaliano baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba, wakiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Katikati), baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Na Benny Mwaipaja, MoFP, Dar es salaam
SERIKALI ya Marekani, kupitia shirika lake la Misaada ya Maendeleo
USAID, imeipatia Tanzania msaada wa dola Milioni 407 sawa na zaidi ya
shilingi Bilioni 895 zitakazotumika kwaajili ya kuendeleza sekta za Kilimo,
Afya, Nishati ya Umeme, Elimu na Utawala Bora, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo kuanzia mwaka 2016/2020.
Hati za Makubaliano hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam, kati ya
Mkurugenzi wa Shirika la USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Msaada huo ni sehemu ya dola Milioni 800, sawa na zaidi ya shilingi Trilion
1.76 ambazo serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga kuipatia
Tanzania ili kufanikisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika
kipindi cha miaka mitano ijayo, wenye lengo la kuiwezesha Tanzania
kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika na serikali ya Tanzania kupitia mfuko
mkuu moja kwa moja wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi zisizokuwa
za kiserikali zinazofanya shughuli zake hapa nchini kufanikisha malengo ya
msaada huo.
Miradi iliyopewa kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI na Kifua
Kikuu, Uzazi wa Mpango, Kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza
utawala wa kidemokrasia, Usimamizi wa Rasilimali za Taifa, na kuwekeza
kwenye sekta ya umeme ili kuimarisha sekta ya viwanda na uzalishaji mali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...