WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imeyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya usajili wao na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa sheria.
Hayo yamesemwa na Marcel Katemba ambaye ni Msajili wa Mashirika hayo, kufuatia tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya NGOs zinazojihusisha na kuhamasisha vitendo vya ushoga nchini.
"Siku za hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayojihusisha na kuhamasisha vitendo vya ushoga
nchini. Tunapenda kuujulisha umma kuwa NGOs zinasajiliwa kutekeleza majukumu
yanayokubalika kisheria na kwamba vitendo vya kuhamasisha ushoga si majukumu
halali yanayopaswa kutekelezwa na NGOs" alisema Katemba.
Aidha, alisisitiza kuwa vitendo vya ushoga havikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi
na sheria za nchi.
Ofisi ya Msajili inaomba wadau na umma kwa ujumla kutoa taarifa
zitakazowezesha kuthibitisha tuhuma tajwa ili hatua stahiki dhidi ya NGOs husika
zichukuliwe. Taarifa zinaweza kutolewa kupitia namba zifuatazo: 022
2110714/0222123143/ 0754391942/0715391942.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...