Na Veronica Simba - GEITA
Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na kufanya shughuli za kiuchumi.
Sambamba na agizo hilo, pia Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.
Aidha, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.
Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.
Maagizo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.
Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na sheria nyingine za nchi.

Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni maafisa kutoka Wizarani.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...