Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa tayari kwa kuanza safari yake ya Jiji kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa rasmi jana.
TRENI ya pili ya Jiji la Dar es salaam imeanza kutoa huduma zake kwa safari  za jiji za kuanzia Stesheni hadi pugu, ambayo itakuwa ikitoa huduma mara 3 kwa asubuhi na mida ya jioni mara 3 ambayo itasaidia sana kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo huku ikiongeza kasi ya uchumi kwa wakazi wa maeneo ya pugu hasa wakiwemo wachuuzi.

Baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo wanaotokea maeneo ya kuanzia kipawa mpaka Pugu, wamepngeza kuanzishwa kwa safari hiyo, kwani itawapunguzia adha ya safari ya muda mrefu njiani na sasa watakuwa wakiwahi katika maeneo yao ya biashara hasa wale wanaofika Soko la Kimataifa la Samaki Ferry kuchukua Samaki, ambapo sasa watachukua usafiri wa Bajaji na kuwahi usafiri wa treni kwa muda uliopangwa.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakigombania kuingia katika mabehewa baada ya kuanzishwa usafiri huo.
Wanafunzi wa Shule Mbalimbali wakiwa ndani ya mabehewa ya Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) katika Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Endeleeni kuboresha usafiri wa jiji

    ReplyDelete
  2. Huyo askari anaedandia behewa huku train ikiwa imeshaanza ku-move ni khatari kufanya hivyo. Nadhani kwa ujumla suala la zima la kiusalama kwa abiria, kabla na baada ya kupanda lizingatiwe, khususan train inapokaribia kuondoka, wahusika wa usalama wa chombo hicho ni vyema wakahakikisha kupo clear pembezoni mote mwanzo hadi mwisho wa mabehewa, then kuruhusu train iondoke, tukijijengea utaratibu huo nadhani tutaimarisha usalama zaidi kuliko hii ya kiholela holela tu huyu anapanda huyu anashuka na yule anadandia, sio utaratibu mzuri. Wahusika lizingatieni na hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...