Na Woinde Shizza, Arusha

Kambi tiba ya GSM Foundation inayotembea nchi nzima kutafuta watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi imemaliza mkoa wa 13 tangu kuanza kwake, na Jumatano hii itaanza kazi mkoa wa Mara ambao utakuwawa 14.

Mkuu wa kambi tiba hiyo, Dk Othman Kiloloma Amebainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha, Dk Kiloloma ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya Muhimbili, MOI alisema kuwa wao kama taasisi walikaa chini na kuona kuna watoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya gharama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho hakina ukweli.

"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 hatujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma

Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kichwa, Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17 aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada.

"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto usisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua, tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.

Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususa ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa.

Alisema anapenda kuwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini hapa Tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...