Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma leo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi alipotembe banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi na wadau mbalimbali nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiangalia vipeperushi na machapisho mbalimbali kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...