Mtangazaji
 wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, 
Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni 
Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Na BMG
Konagamano
 hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kujikomboa kiuchumi ambapo 
wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu 
watakuwepo kuzungumza na wanawake Jijini Mwanza ambapo kiingilio itakuwa
 elfu 40 tu na utapata elimu, burudani pamoja na chakula.
"Atakuwepo
 Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa 
Manjano Foundation ambaye amefanikiwa kwenye biashara, atakuwepo 
Mkandarasi Maida Waziri ambaye amekuwa mkandarasi na amefanikiwa pamoja 
na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni inaitwa Namaingo Agri_Busness 
Agency ambayo inawawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo na 
wengine wengi". Amefafanua Masimba.
Mtangazaji
 wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, 
Mboni Masimba akiwa ndani ya 102.5 Lake Fm Mwanza akizungumzia Kongamano
 la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu 
ndani ya Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Mtangazaji
 wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, 
Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni 
Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...