Moshi, Oktoba 18, 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkaguzi wa polisi Mkoa wa Kilimanjario, Peter Mizambwa , amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha. 

“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mizambwa . 

“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Zauda. 
Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akitoa maelezo katizo kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu katika mkutano na wadau mbali mbali wakiwepo toka vyombo vya usalama na wafanyabiashara wanaofanya kazi na SBL na wafanyakazi wa kiwanda cha SBL moshi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Meneja wa mauzo wa Sbl Mkoani Kilimanjaro Godwin Seleliii akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu iliyofanyika katika mji wa Moshi mkoani kilimanjaro mapema jana. 
Mkaguzi wa polisi Mkoa wa kilimanjaro Peter Mizambwa akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa keampeni ya unywaji kistarabu iliyozinduliwa mapema jana na Sbl katika mji wa Moshi 
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini elimu juu ya unywaji wa kistaarabu katika uzinduzi wa kampeni hiyo mapema jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...