Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu
amezindua kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kuweka huduma ya intaneti kwa njia ya
Wi-Fi katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu katika jiji la Dar es salaam ili kuongeza
fursa kwa watanzania kutumia mawasiliano kwa manufaa ya Taifa katika kuleta
maendeleo.
Mheshimiwa Samia Suluhu alizindua huduma hiyo ya W-Fi katika viwanja vya
Gymkhana katika uzinduzi wa Kampeni ya kupanda miti iliyofanyika jijini la Dar es
salaam Oktoba mosi mwaka huu.
Akizungumza na wakazi waliojitokeza katika viwanja vya Gymkhana, Makamu wa Rais alisisitiza wakazi wa
Dar es salaam kupanda miti na kuitunza ili kuhifadhi mazingira hususani katika
kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, pia alipongeza juhudi za uwekaji wa
huduma ya intaneti kwenye maeneo ya jiji la Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa huduma ya Wi-Fi
ambayo itawekwa katika maeneo ya mkusanyiko ni sehemu ya juhudi za serikali ya
awamu ya Tano kuhakikisha jiji linakuwa na huduma endelevu ya intaneti ambapo
wananchi wataweza kupata huduma hiyo popote walipo, kutumia mawasiliano katika
kujenga Taifa letu kimaendeleo na kupashana habari mbalimbali za kimaendeleo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema kuwa
kutokana na uwezo na uzoefu katika sekta ya mawasiliano TTCL iko mstari wa mbele
katika kuchangia juhudi za serikali katika kuboresha huduma za TEHAMA kwa kuwafikia
watanzania wengi zaidi kupitia huduma hii ya Wi-Fi itakayopatikana katika bustani za
mapumziko jijini Dar Es Salaam.
Pia, Kindamba alisema kuwa “Jitihada hizi kwa kushirikiana na wadau wetu
mbalimbali zitaendelea na kuhakikisha kuwa sehemu nyingi zenye mikusanyiko ya watu
wengi wanapata huduma hii ya Wi-Fi. Mathalani maeneo ya haya ni vituo vikubwa vya
mabasi, viwanja vya ndege, vyuo, majengo makubwa yenye wakazi wengi, viunga vya
mapumziko, viwanja vya mpira kwa kuwa dunia ya leo mawasiliano ni chachu muhimu
katika kuboresha maisha yetu, na kupashana habari na matukio muhimu”
Aidha, mpango huu wa Wi-Fi utakua endelevu kufikia lengo la kujenga miji na majiji
yetu kwa kiwango cha “Smart City” ili pia kuimarisha ulinzi na usalama wa miji, watu na
mali zao.

![]() |
Mkuu wa Kanda Kibiashara wa Dar es salaam wa TTCL,
Jane Mwakalebela na wadau wakipanda miti katika viwanja vya Ghymkhana,
Dar e salaam.
![]() |
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Bw Waziri Waziri Kindamba
akiwa pamoja na wanafunzi wa Skauti, viwanja vya Ghymkhana
![]() |
Wafanyakazi wa TTCL
wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema, baada zoezi la kupanda kukamilika katika viwanja vya Ghymkhana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwa njia ya
Wi-Fi kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya intaneti ya Wi-Fi
inapatikana bure kwa wakazi wa jiji Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Sophia Mjema akishiriki zoezi
la kutumia Wi-Fi katika banda la TTCL , ambapo TTCL ilikuwa ikitoa
huduma ya intaneti Bure.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba na
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo, Peter Ngota wakipanda miti katika
viwanja vya Ghymkhana, ambapo TTCL iliweka huduma ya intaneti
bure ya Wi-Fi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...