Vijana wa Kitanzania waliopata bahati ya kwenda kujifunza masuala mbalimbali kupitia programu ya kubadilisha vijana na nchi ya Ujerumani wametakiwa kuweka uzalendo mbele kwa nchi yao na kurudi nyumbani kuitumikia.
Vijana wa Kitanzania wataungana na wenzao katika program ya kubadilishana vijana na nchi ya Ujerumani kujifunza masuala mbalimbali yahusuyo lugha, utamaduni na ufundi stadi. 
Tanzania ilishinda programu hiyo kupitia asasi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition (TYC) baada ya kutuma andiko lake sambamba na mataifa mengine Afrika ambapo nchi tatu tu Tanzania ikiwa mojawapo ndizo zilizoshinda.
Mpango huo wa kubadilisha vijana ni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 na vijana watakuwa wanaenda ujerumani kujifunza kwa muda wa mwaka mmoja mmoja.
Akizungumza wakati wa kongamano la wadau lililotayarishwa na TYC mwishoni mwa wiki, Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema vijana watakaokwenda Ujerumani wanatakiwa kujifunza kwa bidii, kupata maarifa mapya na kutengeneza mahusiano mapya kwa faida yao na nchi kwa ujumla.
“Serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda na inategemea sana vijana ili kuendelea,” alisema na kuongeza kuwa ujuzi watakaopata ni wa muhimu na unategemewa.
Katika kongamano hilo, asasi ya TYC ilikutana na asasi nyingine kutoka Benin na Afrika ya Kusini kujadili namna ya kutekeleza programu hiyo.
Alisema NEEC ilishiriki kuanzia mwazo wakati programu hiyo ilipokuwa ikizinduliwa ujerumani na kwamba serikali imejipanga kusimamia vizuri programu za kubadilishana vijana na Ujerumani na nchi nyingine kwa faida ya taifa.
Mkurugenzi wa TYC, Bw. Lenin Kazoba alisema warsha hiyo ilikuwa ya wadau ambao walijadili namna bora vijana wa mataifa hayo watakavyoshiriki katika programu hiyo.

Asasi hiyo sasa itawakilisha nchi za Afrika Mashariki, wakati vijana toka Afrika Kusini watawakilisha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakati nchi ya Benin itawakilisha Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Programu hiyo ilianzishwa baada ya serikali ya Ujerumani kukubaliana na Umoja wa Afrika (AU) kushindanisha nchi za Afrika na hatimaye asasi kutoka nchi hizo tatu kushinda.
Asasi ya TYC inajumuisha vijana wa sekondari, vyuo vya ufundi stadi, vyuo vikuu na watu wenye mahitaji maalum.
Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kushoto) akizungumza wakati wa kongamano lililotayarishwa na asasi ya kiraia ya Tanzania Youth Coalition (TYC) iliyoshinda nafasi ya mpango wa kubadilishana vijana na nchi ya Ujerumani.  Mpango huo wa miaka mitatu unaoanza mwaka 2017 unahusisha pia nchi za Benin na Afrika ya Kusini.  Kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha vijana, Umoja wa Afrika, Bi. Prudence Nonkululeko Sigwane na Mkurugenzi wa TYC, Bw. Lenin Kazoba (katikati).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...