WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Gerson Lwenge, ameiagiza Kampuni ya Serengeti Limited
kukamilisha mradi wa uchimbaji visima 20 vya maji vya Kimbiji na Mpera
kwa muda waliokubaliana, vinginevyo itabidi ilipe gharama za
ucheleweshaji kama itashindwa.
Alisema serikali haitavumilia
kuona mradi huo wenye manufaa makubwa kwa Jiji la Dar es Salaam
unachelewa kukamilika, kwa sababu unahitajika kuhudumia wananchi kwa
kuwapatia huduma ya majisafi na salama.
Waziri Lwenge alitoa
agizo hilo mwishoni mwa wiki, baada ya kufanya ziara ya kukagua
utekelezaji wa mradi huo mkubwa uliopo Kigamboni, Dar es Salaam ulioanza
kutekelezwa tangu mwezi Machi, 2013.
Alisema mradi huo
utagaharimu zaidi ya Sh. bilioni 18, na serikali imeshalipa kwa
mkandarasi zaidi ya Sh. bilioni 13, na ulitegemewa kukamilika ifikapo
Desemba mwaka huu, lakini utachelewa kutokana na changamoto mbalimbali
alizotaja mkandarasi huyo.
“Pamoja na changamoto alizozitaja
mkandarasi, hatutakubali utekelezaji wa mradi huu uendelee kuchelewa,
mkandarasi inabidi aongeze kasi ili tumalize kero ya wananchi wa
Kigamboni, Mkuranga na Dar es Salaam yote, ambao kwa muda mrefu wamekuwa
wakisubiri mradi huu, hatutavumilia uchelewaji zaidi na itabidi walipie
gharama endapo watashindwa”, alisema Inj. Lwenge.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akipokea maelezo ya ramani ya mradi wa uchimbaji visima vya Kimbiji na Mpera kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa mradi, Injinia Charles Kaaya. 
Mashine ikiendelea na kazi ya uchimbaji kisima Kimbiji. 
Baadhi ya mafundi wakiwa eneo la kazi Kimbiji. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Serengeti, Mehrdad Talebi (kushoto), Mhandisi Mkazi wa mradi, Charles Kaaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Archad Mutalemwa na Mkurugenzi wa Maji Mijini, Mhandisi Dkt. Justus Rwetabula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...