Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo amewashauri wasanii wa filamu nchini kujiendeleza kielimu ili kuongeza weledi na kutengeneza filamu zenye ubora.

Akiongea na uongozi wa Kituo cha Radio na Televisheni cha East Afrika leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa chombo hicho kina nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa wasanii hususani namna ya kuandaa Filamu zenye bora kwa kuwa wako mstari wa mbele katika kuonyesha kazi za tasnia hiyo. 

“Kituo chenu kina nafasi kubwa zaidi ya kushawishi wasanii kutengeneza filamu bora kwa kuwa mmekuwa mkiwapatia fursa ya kutangaza filamu hizo pamoja na kuzionyesha ndani na nje ya nchi hivyo ni muhimu kuwakumbusha kuzingatia ubora wa filamu .”Alisema Bibi Joyce.

Aidha ameongeza kuwa vyombo vya Habari ni nguzo muhimu katika kuendeleza tasnia ya filamu hapa nchini hivyo ni budi kwa wasanii kuhakikisha wanatengeneza Filamu bora ambazo zitapata nafasi ya kuonyeshwa katika vyombo hivyo kwa maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa vipindi vya televisheni wa East Afrika Bi Lydia Igarabuza ameipongeza Bodi ya Filamu kwa kufanya maboresho katika tasnia ya Filamu nchini na kuishauri kutoa elimu zaidi kwa wasanii katika kufuata Sheria ya Filamu na michezo ya kuigiza kabla ya kutengeneza filamu zao.

“Naipongeza Bodi ya Filamu kwa juhudi mnazofanya katika kuboresha tasnia hii na msichoke kutoa elimu hiyo kwani wasanii wetu bado wanahitaji elimu ya filamu na sheria zake kwa ujumla.Alisema Bi Lydia.

Bodi ya Filamu imejidhatiti katika kuhakikisha tasnia ya Filamu inakuwa kwa kutengeneza bidhaa bora ambapo imekuwa ikitoa mafunzo kuwajengea uwezo wanatasnia hao .
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Wa kwanza kushoto ) akizungumza na uongozi wa East Afrika Televisheni na East Afrika Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa vipindi vya EATV Bi Lydia Igarabuza.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji wa EA Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji wa EATV alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa vipindi vya East Afrika Televisheni Bi Lydia Igarabuza (wa kwanza kulia) akimueleza jambo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...