Wakati
msimu mpya wa kilimo ukiwa unatarajiwa kuanza, Kampuni ya Mbolea Tanzania
(Tanzania Fertilizer Company – TFC) imeanza zoezi la kusambaza mbolea ya ruzuku
kwenda katika mikoa inayotarajia kuanza msimu wa kilimo wa 2016/2017.
Akiongea
na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Mbolea Tanzania, Bwana Salum Mkumba amewataka wakulima kujiandaa kupokea mbolea
ya ruzuku ambayo imeanza kusafirisha tangu jana tarehe 7/11/2016 kutoka kwenye
maghala ya Kampuni hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam kwenda Mikoa 20 ya
Tanzania Bara.
Bwana
Mkumba amesema kuwa kwa zoezi la kusambaza mbolea hiyo ya ruzuku, litahusisha
kiasi cha tani 32,300 (Tani elfu thelasini na mbili na mia tatu) ambazo
zinaigharimu Serikali fedha kiasi cha shilingi bilioni 12 ambapo mkulima
atapaswa kununua mfuko wa mbolea ya kupandia au kukuzia wa kilo 50 kwa shilingi
30,000.
Bwana
Mkumba aliongeza kuwa mbolea hiyo imeanza kupelekwa katika Mkoa wa Katavi na
Mikoa minginge ya Nyanda za Juu Kusini, Mikoa hiyo matumizi ya mbolea yapo juu
na kwamba zaoezi hilo litaendelea kwenda Mikoa mingine kwa kutumia usafiri wa
Reli na Barabara mpaka kukamilisha zaidi ya tani 32,000 zilizokusudiwa.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Pembejeo, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi,
Bwana Shanil Nyoni amesema, lengo la Serikali ni kuiwezesha Mikoa 20 kupata
mbolea hiyo na ndivyo itakavyokuwa na kwamba Mkoa wa Katavi na Rukwa inaanza
kupata mbolea hiyo kwa sababu, msimu wa kilimo unaanza hivyo itawafikia kwa
wakati.
Bwana
Shanil ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuwasaidia wakulima wasio na uwezo
wa kumudu kununua mbolea na kwa utaratibu unaanza kwa kuwatambua wakulima
kuanzia katika ngazi ya Kijiji wenye sifa
ya ukaazi wa eneo hilo, mwenye eneo la kulimia mahindi kuanzia ekari moja, na awe
mkulima aliyetayari kupokea utaalam wa matumizi ya pembejeo hizo, ikiwemo
mbolea na mbegu bora na awe tayari kuchangia gharama kidogo na kuongeza kuwa
kwa kuanzia mpango huu umelenga kuwafikia wakulima laki tatu.
Aidha
Bwana Nyoni amewataka wakulima kuondoa hofu ya kuwa mbolea hizo zinadumaza
mazao na badala yake zinaongeza tija na uzalishaji kwa kuwa zimefanyiwa utafiti
kabla ya kuwafikia wakulima kulingana na udongo na aina ya mazao.
Mkurungezi
Msaidizi wa Pembejeo za Kilimo Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvvi Bwana Shanil
Nyoni akizungumza na Waandishi wa Habari
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania Bwana Salum Mkumba akisema jambo
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.
Baadhi ya
Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) wakipakia mifuko ya
mbolea ya ruzuku tayari kwa kusafirishwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...