Naibu
Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu
wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi leo amezindua tamasha la tano ya watu
wenye ulemavu nchini, Tamasha lililoandaliwa kwa udhamini wa Shirika
lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society, lililofanyika
katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
Dk. Posi amebainisha katika Tamasha hilo kuwa, serikali ipo karibu na watu wenye ulemavu na kwamba sheria iliyopitishwa mwaka 2010, kuhusu watu wenye ulemavu imepitishwa na kwamba ni jukumu la jamii nzima kushirikiana katka kutoa haki sawa kwa wananchi wote wakiwemo walemavu.
Dk. Posi alifafanua kuwa, changamoto zinazowakabili walemavu hapa nchini ni nyingi lakini pia serikali inazitambua, inazichambua na inazifanyia kazi kwa kadri uwezo unapopatikana.
Kabla ya hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society, Fransis Kiwanga alifafanua kuwa, shirika analoliongoza kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha walemavu hapa nchini, liliona ni busara kuchangia kuwepo kwa tamasha hili na kwamba ni faraja kwa shirika hili kuona maisha na hali ya walemavu hapa nchini inabadilika.

Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi, akizungumza wakati akizindua tamasha la tano ya watu wenye ulemavu nchini, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa kwa udhamini wa Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society. Picha na Muhidin Sufiani
Mkurugenzi wa Shiriki lisilo la Kiserikali la Foundation for Civil Society, Francis Kiwanga, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Tamasha hilo kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam,leo. Picha na Muhidin Sufiani
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani.
PICHA ZAIDIBOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...