Mkuu
wa Wilaya ya Arusha ametoa angalizo kwa wananchi wote kuhusu tahadhari ya
mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeripotiwa kuwepo katika Mikoa
mbalimbali na maeneo ya jirani na Wilaya hii.
Akizungumza kwenye kikao maalumu na watendaji wa Kata,
Maafisa Afya pamoja na wadau wa Afya Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Alexander Mnyeti ameelezea hatua ambazo
Serikali ya Wilaya imechukua hadi hivi sasa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa kuwa
ni:
-
Kuandaa
kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa watakaojitokeza –ipo katika Kituo cha Afya
Levolosi
-
Kuagiza dawa
na vifaa tiba kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa
-
Kusambaza mabango, vipeperushi na miongozo katika vituo vua kutolea huduma za afya,
Ofisi za Kata na mitaa pamoja na maeneo ya mikusanyiko
-
Kufanya
kikao na wadau wote na kuunda timu ya usimamizi wa mlipuko wa kipindupindu.
Kupitia kikao hiki kwa kauli moja wajumbe walikubaliana hatua za
kuchukua ili kupambana na mlipuko:
-
Kuhakikisha
upatikanaji wa maji safi kwenye maeneo
yote yenye uhaba wa maji
-
Kuchukua
Sampuli za maji katika Kata za pembezoni
-
Kupiga
marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa,vyakula barabarani na pombe za kienyeji
-
Kutembelea
kaya na kukagua uwepo wa vyoo na matumizi yake
-
Kugawa
vidonge vya Kutibu maji kwenye kila Kaya
-
Kuwachukulia
hatua wote watakaokiuka wa kanuni za Afya
Pia wananchi walishauriwa kujikinga na ugonjwa huu kwa njia
zifuatazo;
-
Kunywa maji
yaliyochemchwa au yaliyowekewa dawa ya kuua vimelea
-
Kula chakula
cha moto kilichotayarishwa katika hali ya Usafi.
-
Kunawa
mikono kwa sabuni na maji ya kutitirika (usinawe ndani ya chombo).
-
Kuhakikisha
matumizi bora ya choo na kinyesi cha watoto wadogo kitupwe chooni
-
Kuepuka kula
matunda bila kuyaosha na kunywa juisi na vyakula vinavyouzwa kiholela.
IMETOLEWA NA
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
17 Novemba
,2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...