Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAKIMBIZI wamekuwa wakiishi maisha ya kambini kutokana na sheria pamoja na mikataba hali ambayo imesababisha kukosa fursa ya kuzalisha katika taifa walilopo.
Akizungumza na waandishi katika mafunzo yaliyoandaliwa na Asylum Access, Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Juliana Masabo amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo imekuwa ikipata wakimbizi ambao wanaishi katika makambi lakini kutokana na sheria ya wakimbizi inaelekeza kuishi katika mazingira hayo bila kujishughulisha na uzalishaji wowote.
Amesema wakimbizi wana haki sawa kama binadamu wengine hivyo sheria zinahitaji kufanyiwa maboresho kutokana na mazingira yaliyopo, wanatakiwa kuangaliwa kuwa sehemu ya watu ambao wanaweza kuzalisha
Dk. Juliana amesema kuwa kuna watu ni wataalam lakini wamekuwa wakimbizi lakini hawawezi kuajiliwa katika taifa walilopo kutokana na sheria kuwabana ya ukimbizi hivyo utaalam walio nao unabaki katika makambi usio wa uzalishaji.
Nae Wakili na Mtetezi wa Haki za Wakimbizi, Veronica Hollela amesema kuwa kunahitajika kufanyika kwa uboreshaji wa sheria ya wakimbizi ili kuweza kuishi kwa huru na kufanya kazi kama raia wengine na kuwa faida ya nchi kuongeza uchumi.
Veronica amesema maisha ya wakimbizi ni magumu kutokana na kukaa sehemu moja ambayo hawana uzalishaji na kuishi kwa kutegemea misaada.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Boniventure Rutinwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu kutoa taarifa zinazohusu wakimbizi na changamoto zao , mafunzo hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Aslum Access yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Juliana Masabo akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya sheria zinazohuusu wakimbizi mafunzo hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Aslum Access yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
picha wa pamoja ya wakufunzi wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya wakimbizi mafunzo hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Aslum Access yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...