MWANAMUZIKI wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Darassa na Roma,
kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka
Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la
Nichane Nikuchane.
Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar,
leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni
kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.
Akizungumza na
mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha
wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live
kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya
miujiza kila ninapopanda jukwaani.”
Naye Meneja wa Mkuu wa
Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo,
Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti,
kama tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa
kwenye Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda
kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye
siku hiyo."
Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu
wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000,
mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali
ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”
Mbali na wakali
hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni
pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature,
Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

Darassa akigonga shoo ya bure Viwanja vya Karume leo.


Mashabiki wakisukuma gari la Darassa.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa shoo ya R.O.M.A na Darassa, Abdallah Mrisho akitoa ufafanuzi kwa wanahabari waliokuwepo Viwanja vya Karume jijini Dar, leo kuhusu shoo hiyo. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...