Na Amina Kibwana,Globu ya jamii
Halmashauri
ya manispaa ya kinondoni imezindua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji
wa jiji la dar es salaam kwa kusaini mkataba wenye thamani ya bilioni 22
na mkandarasi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.
Akizungumza
na waandishi wa habari maeneo ya makumbusho kata ya kijitonyama
leo,Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sitta amesema kuwa mpango
wa mradi huu unalenga kuboresha miundombinu ya barabara ambayo
itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na
kuongeza thamani ya makazi ya watu pamoja na kupinguza umaskini.
"Katika
uboreshaji wa miundombinu barabara zitajengwa kwa lami nzito na huduma
nyingine za watumiaji wa barabara kama maeneo ya waendao kwa miguu,taa
za barabarani,mitaro ya majia pamoja na alama za vivuko ambavyo
vitambadilisha sura ya manispaa ya Kinondoni na jiji la Dar es Salaam
kwa ujumla."
Aidha meya ametaja barabara
ambazo Zitahusika katika mpango huu ni pamoja na soko la makumbusho
km1.45,MMK km 0.9,Nzasa km 1.25, Viwandani km 1.68 na Tanesko soko la
samaki ambazo zitajengwa ndani ya mwaka mmoja na kwa kiwango cha juu.
Kwa
upande wake mkandarasi kutoka Estim Construction Jagdish Bhudia amesema
kuwa watajenga barabara kwa kiwango kinachotakiwa kama kwa kutumia lami
nzito ili ziweze kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.
Hata
hivyo mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni ameongeza kwa kuwataka
wanachi wote wa manispaa hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi
huu ambao unalenga kuboresha miundombinu na kuimarisha huduma za
kiuchumi, kibiashara na kijamii.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni Benjamini Sitta akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kusaini mkataba huo jijini dar es salaam,kushoto ni mhandisi wa manispaa hiyo Abdul Digaga
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mapema Leo Jijini Dar es salaam.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...