Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Ally Hapi amezungumza na vyombo vya habari leo na kueleza umma kuwa kampuni ya Zantel imetii agizo alilotoa la kulipa mapato ya zaidi ya milioni 687 yatokanayo na mkataba ulioingiwa na manispaa ya Kinondoni mwaka 2009 uliogubikwa na harufu ya ufisadi katika utekelezaji wake.
Mkataba huo ambao tangu usainiwe mwaka 2009 kati ya manispaa ya Kinondoni na kampuni ya Zantel, kampuni hiyo haikuwahi kulipa mapato husika kwa manispaa hiyo kwa mujibu wa mkataba.
Aidha, mkataba husika uliibwa katika nyaraka za manispaa hiyo na hivyo mapato hayo kutokuwa na ushahidi wa kuyadai.
Mapema wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi alitinga ofisi za kampuni hiyo akiwa na mkataba husika huku akiambatana na Kamati ya ulinzi na usalama na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Aron Kagurumjuli na kuutaka uongozi wa Zantel kulipa mapato hayo ya kimkataba ndani ya siku 7.
Kampuni ya Zantel imelipa fedha hizo tarehe 21 Disemba 2016 ndani ya wakati waliopewa kiasi cha zaidi ya milioni 687.
Baada ya kulipwa fedha hizo Hapi ameeleza kuwa ametoa maelekezo na manispaa imeanza kujipanga kwa mujibu wa taratibu zake kuzipeleka fedha hizo katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari ambapo wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa Madarasa 79 ya sekondari, hali inayowafanya wanafunzi zaidi ya 3169 waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kukosa nafasi.
Fedha hizo zitawezesha jumla ya  madarasa mapya 40 kujengwa Kinondoni.
“Tutahakikisha tunawabaini wote waliohusika kula njama za kuhujumu serikali na kuuficha mkataba huo kwa muda wa miaka saba..." alisema.
Hapi  alisema kutokana  na ulipaji huo Manispaa ya Kinondoni kwa  sasa tayari imeshawapa  risiti ya malipo   ya fedha hizo ambapo zililipwa Disemba  21, mwaka huu.
Kaimu Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa kampuni zilizoingia mkataba na manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam miaka ya nyuma kuhakikisha wanalipa mapato yote ya serikali na kwamba wahusika watasakwa popote walipo hata kama mikataba husika wameiiba kifisadi katika mafaili ya manispaa kwa kushirikiana na watumishi wasio waadilifu.
Katika hatua nyingine, Hapi amelipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya kazi nzuri ya kudhibiti na kuhakikisha kunakua na usalama wa kutosha wakati wa sikukuu za Christmas. Amewatakia wananchi wote wa Dar es Salaam kwa niaba ya serikali ya Mkoa sherehe njema za mwaka mpya zenye amani na baraka na kwamba vyombo vya dola jijini Dar es Salaam vimejipanga vema kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...