Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi, Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya mchango uliotolewa na Ubalozi wa Korea kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera mwezi Septemba, 2016 na kusababisha madhara makubwa, Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mhe.Song Geum Young
Waziri Mahiha akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani elf 50 (shillingi millioni 108) kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Song.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo y Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiratibu hafla hiyo.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hafla ya makabidhiano, Kutoka kushoto ni Bw. Halmenshi Lunyumbu, Bw. Assah Mwambene, Bw. Ally Kondo na Bw. Freddy Maro.
Hafla ya makabidhiano ikiendelea.
Picha ya pamoja.
Na Amina Kibwana, Glogu ya Jamii.
Serikali ya Tanzania imepokea pokea msaada wa dola za kimarekani 50,000 (Dola elfu hamsini) kutoka ubalozi wa jamuhuri ya Korea kwa ajili ya kukabiliana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, ili kuweza kurekebisha Miundombinu, makazi ya watu pamoja na shule.
Akizungumza wakati kupokea msaada huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kitaifa, Dk. Augustine Mahinga amesema serikari ya korea ni mdau mkubwa hasa katika misaada ya kimaendeleo, kiuchumi , ustawi wa jamii na katika misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa hospitali ya mloganzila na chanika.
“Tumekuwa tukipokea misaada mbalimbali kutoka kwa marafiki lakini huu ni mchango wa hivi karibuni kutoka kwa wenzetu wa korea ambapo leo nimepokea hundi hii kwa niamba ya waziri mkuu na serikali ya Tanzania kwa ujumla.”
Hata hivyo Dk mahinga aliongeza kuwa hundi hiyo ni zawadi kubwa kwa wanachi wetu hasa wa kagera pamoja na kutoa shukrani zake kwa balozi wa korea na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake balozi wa jamuhuri ya korea, Song Young amesema kuwa kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu Korea imeamua kutoa msaada huo, Korea imeamua kwamba katika kuendeleza ushirikiano wa maendeleo na nchi za Afrika Tanzania itapewa kipaumbele na kuwa ni chi ya kwanza kwa Afrika ili kudumisha ushirikiano kati ya Jamuhuri ya Korea na Tanzania.
huu ni mwaka wa 25 tangu Jamhuri ya Korea kuanzisha ubalozi wao nchini Tanzania,hivyo ili kudumisha ushirikiano huo, Serikali ya Tanzania kupitia Rais wake Dk. John Pombe Magufuli nayo inatarajia kuanzisha ubalozi wake huko Soul, mji mkuu wa korea kusini mapema mwaka 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...