Na Woinde Shizza,Arusha

Chama cha soka Mkoa wa Arusha (ARFA) kimefanikiwa kupata uongozi mpya baada ya uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Monduli ambao watakaa madarakani kwa miaka minne.

Katika uchaguzi huo uliokuwa unawaniwa nafasi kumi, ulionekana mgumu kwa nafasi mbili pekee ile ya Mwenyekiti pamoja na nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF,ambapo wagombea walikua wawili wawili.

Waliofanikiwa kupita katika uchaguzi huo kwa nafasi ya mwenyekiti ni Peter Temu aliyemshinda Omary Walii kwa kura 13 kwa 6, Katibu mkuu Zakayo Mjema aliyepata kura 18, katibu msaidizi akipitaNassoro Mwarizo.

Nafasi ya Mweka hazina ikienda kwa Omary Nyambuka, Huku nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Issa Hamisi alimshinda Athumani Mhando kwa kura 13 kwa 8, na nafasi ya kamati tendaji ya ARFA ikienda kwa Soud Abdy.

Washiriki ambao ni wajumbe wa vyama vya soka kutoka Mkoani hapa waliojitokeza ni kutoka Arusha Mjini, Monduli, Arumeru, Karatu, Longido, FRAT ambao walifanya jumla ya wajumbe 19 waliopiga kura.

Huku nafasi ya wajumbe watatu wa kamati tendaji iliyopata mtu mmoja na mwakilishi wa vilabu ambazo hazajajazwa utafayika uchaguzi mdogo baada ya siku 90 kupita alisema katibu wa kamati ya Uchaguzi Seleimani Kirua

Katibu mkuu mpya wa ARFA Zakayo mjema akiongea na gazeti hili alisema wameingia madarani huku kukiwa na deni kubwa la kuitendea haki Arusha ili kuweza kurudisha timu ligi kuu.

" Kwanza nashukuru nimechuguliwa kwa idadi kubwaya kura na hii ni dhahiri wajumbe wameniamini na nitahikisha tunashirikiana kwa pamoja na wilaya zetu katika kuhakikisha soka la mkoa huu linarejea kama ilivyokuwa zamani,"alisema Mjema.

Mwenyekiti mpya Peter Temu aliwasihi wadau wa soka wawe na matumaini kuwa mpira utarejea kulingana na safu mpya yenye morali ya wa kusaidia na kuendeleza mpira.
Mwenyekiti mpya wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha (ARFA) Peter Temu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...