Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Hapi amesema kuwa baadhi ya vituo vya mafuta havina ubora wa mazingira licha ya kuwa na majina makubwa.

Hapi ameyasema hayo leo wakati uzinduzi wa maboresho ya kituo cha mafuta cha Total kilichopo maeneo ya Sokota barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, amesema vituo vya mafuta vinahitaji kuwa mazingira bora kutokana na huduma wanayoitoa.

Amesema Total imejikita katika uhifadhi wa mazingira kwa kutengeneza vituo bora vya mafuta tofauti vituo vingine ambavyo havisadifu na majina ya kampuni na kuwaasa kuboresha vituo vyao ili kuendana na mazingira ya kisasa.

Hapi amesema kuwa vilanishi vinavyopatikana katika kituo hicho kujenga kiwanda nchini kutokana na kuwepo kwa magari mengi na yatazidi kuongezeka kutokana na viwanda vinavyojengwa nchini.

Katika uzinduzi huo ameomba mafuta lita 10,000 kwa kampuni ya Total kwa ajili ya kutumia katika uchongaji wa barabara za manispaa ya Kinondoni ambapo alikubaliwa kupewa lita hizo.

Amesema kuwa kuna kampuni imejitolea kutoa mitambo ya kufanya kazi hiyo lakini waliomba mafuta nijitegemee kwa kupata mafuta kwa hayo kazi itafanyika.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Total, Tarik Moufaddal amesema kituo cha mafuta kuboreshwa kuendana na wakati wa sasa kutokana na huduma wanayoitoa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alli Hapi pamoja na Mwenyekiti wa Total Afrika Mashariki na Kati, Jean Christian Bergeron(wa pili kutoka kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alli Hapi akipeana mkono na Mwenyekiti wa Total Afrika Mashariki na Kati, Jean Christian Bergeron kuashiria uzinduzi cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alli Hapi akizungumza wakati uzinduzi wa kituo cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Total, Tarik Moufaddal(kulia) akizungumza katika uzinduzi wa ya kituo hicho.


Sehemu ya wafanyakazi wa kituo cha mafuta Total wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...