Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amewapongeza uongozi wa benki ya DCB kwa kuweza kuwasogezea huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" kwani kwa hatua hiyo ni wanakuwa miongoni mwa benki zinazoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia za kisasa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya Sitta amesema kuwa kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki na zaidi anautaka uongozi wa bodi ya DCB kuongeza juhudi na ubunifu katika kuileteta mafanikio zaidi siku zijazo na kuendelza sifa nzuri iliyopatikana.

Ameongeza na kusema kuwa, kuna changamoto ,mbalimbali katika sekta za kibenki zinakabiliana nazo ila ametoa ushauri kwa manispaa za Dar es salaam kutumia benki hiyo katika shughuli zao za kibenki ili kuiwezesha kupata amana za kudumu na zaidi amesisitiza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wataendelea kuwa mstari wa mbele kutumia DCB kwani wameweza kufaidika na gawio la kila mwaka.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka amemshukuru mstahiki  meya kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa huduma ya kipesa ya 'DCB Jirani' na "DCB Pesa" na kumshukuru kwa hatua nzuri ya Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kwa kukubali kupitisha mfuko wa mkopo ya  wanawake na vijana katika benki ya DCB.

Msimbachaka ameziomba manispaa hizo kuleta fedha za asilimia 10 ya mapato yao zinazotengwa na kila manispaa kwa ajili ya mfuko huu ili benki iendelee na mpango wake wa kuwakopesha wajasiriamali kwa niaba yao.

Akieleza kuhusiana na DCB Jirani, Msambichaka amesema kuwa kwa kutumia huduma hii ya kisasa wateja wa DCB wanaweza kufaidika kwa kupata huduma za kibenki katibu na mahala anapoishi bila kufuata tawi la benki hiyo, kwa upande wa DCB Pesa mteja ataweza kutumia simu kulipia huduma mbalimbali kama Dawasa, Luku, DSTV, kununua muda wa maongezi, kukopa mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuendeleza biashara na pia wafanyakazi wataweza kutumia kwa kuomba nusu ya mshahara.

Mbali na hilo, pia DCB waliweza kuwakabidhi zawadi zao wateja waliofanikiwa kushinda kwenye droo ya awali ya Kampeni ya kufungua na kuweka amana na DCB benki ambapo washindi 20 waliweza kukabidhiwa zawadi zao za Tshirt, wawili walikabidhiwa simu za mkononi aina ya Smartphone na wengine watatu walipatiwa ada ya shule kwa ajili ya watoto.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta (katikati) akikata utepe wa kuzindua  huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" sambamba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa (kushoto).
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka (katikati) wakizindua magari ya DCB Jirani na DCB Pesa  jana Jijini Dar es salaam, pembeni ni  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa.

Wafanyakazi wa Benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta jana Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...