EFM redio imejinyakulia tuzo NNE usiku wa kuamkia
jana katika tuzo za Tanzania Leadership Awards (T.L.A 2016) kwa vipengele vya
Redio bora ya mwaka, Kampuni bora kwa ubunifu, kampuni inayokua kwa kasi pamoja
na tuzo ya mwandishi bora ya mwaka ambayo imekwenda kwa mtangazaji wa kipindi
cha uhondo katika redio hiyo bibie Dina Marios.
Hafla ya ugawaji tuzo hizo ilifanyika siku ya tarehe
27/1/2017 katika ukumbi wa Hyatt regency hotel jijini Dar es salaam, ambapo
redio hiyo iliwapatia heshima kubwa wasikilizaji wake kwa kuondoka na tuzo
hizo.
Ni mwaka wa pili mfululizo kwa redio hio kuchukua tuzo za
Tanzania Leadership Awards ambapo tuzo ya kwanza waliipata mwaka jana kwa
kipengele cha redio bora ya mwaka.
Ni takribani miaka mitatu sasa tangu redio hii ianzishwe na
imejipatia umaarufu mkubwa kwa kuutangaza muziki wa singeli, na kujihusisha na
mambo mbalimbali ya kijamii kupitia matamasha,vipindi na kampeni mbalimbali
kama vile kupanda miti (mti wangu), kuanzisha vikundi vya mazoezi (efm Jogging
club), kampeni za afya, kuhamasisha jamii kujikita katika shughuli za
ujasiliamali, pia kutatua matatizo katika jamii kwa lengo la
kujiweka karibu na jamii nzima .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...