Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Pastory Athanas akikabiliana na Mabeki wa timu ya Azam Fc, katika kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara duru la pili, unaoendelea kuchezwa hivi sasa katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam FC yaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Mshambuliaji John Bocco.
Beki wa Azam Fc, Aggrey Moris akiondosha hatari iliyokuwa imeelekezwa langoni kwake.
Kipa wa Simba, Daniel Agyei akinyaka mpira kwa umaridadi kabisa huku Beki wake, Method Mwanjale akimzuia Mshambuliaji wa Azam, John Bocco asiweze kuufikia mpiara huo.
Beki wa Simba, Mohammed Hussein akisepa na kijiji cha Azam, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara duru la pili, unaoendelea kuchezwa hivi sasa katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam FC yaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Mshambuliaji John Bocco.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...