Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika jana 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuwatunuku Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada wahitimu hao jana 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo jana 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...