Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja
Kueleka mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi baina ya Azam
na Simba makocha wa pande zote mbili wameanza kutambiana kila mmoja akijinadi
kuwa ana uwezo wa kumfunga mwenzake ndani ya dakiika 90.
Fainali hiyo inayofanyika kesho kwenye uwan ja wa Amani inawakutanisha
timu hizo zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo Azam wakiwatoa Jang'ombe Taifa kwa
goli 1-0, Simba wakiwatoa Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2.
Kocha msaidizi
wa Simba Jackson Mayanja amejigamba kwa kusema kuwa mechi kati yao na Azam ni
mechi ya fainali na ina utofauti mkubwa sana na mchezo uliopita wa watani wao
wa jadi na walifanikiwa kuwaondoa kwa mikwaju ya penati.
Ameweka wazi kuwa mechi
hiyo itarajiwa kuwa ni moja ya mchezo wa kukata na shoka kwani silaha zoet zipo
kamili na zinajiandaa kikamilifu kabisa.
“Maandalizi yapo vizuri kabisa, tuna
majeruhi wawili ambao ni Blagnon pamoja na Mohamed Ibrahim kwani hatuna uhakika
kama anaweza kucheza ila wengine wote wako vizuri,”
Kocha wa muda wa Azam
Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kupambana na anataka
kuhakikisha analichukua kombe la Mapinduzi kwani timu nzima inajiamini na
watashuka dimbani kupambana.
Pia amesifu safu yake ya ushambuliaji kutokuruhus
goli hata moja mpaka wanaingia hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup 2017.Cheche
amejigamba kuwa anaifahamu vizuri Simba toka anacheza na pia amecheza nazo
nikiwa mchezaji na sasa hivi ni mwalimu najua najua jinsi ya kuzikamata.
Azam
imelichukua kombe la Mapinduzi mara mbili (2012 na 2015) tangu ilipoanza
kushiriki michuano hiyo wakati Simba tangu 2007 wamelibeba mara tatu (2008,
2011 na 2015)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...