Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kanali Marco Gaguti amewaonya wakimbizi wenye historia ya uhalifu nchini Burundi wanaoingia Nchini Tanzania, kwa kigezo cha kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa kuhofia wasikamatwe kwa uhalifu walioufanya Nchini mwao, kuwa ikibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha, Gaguti aliuomba uongozi wa Nchi ya Burundi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya hiyo iliyopo Mpakani, kuwabaini waomba hifadhi hao wanaoingia Nchini kwa kukimbia uhalifu walioufanya Nchini mwao na kuja kuendeleza vitendo hivyo wanapo ingia Nchini.
Hayo yalibainika jana wakati wa Kikao cha majadiliano baina ya Mkuu huyo na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, alipokuwa akihoji ni kwanini wahamiaji wengi wanaongezeka Nchini wakidai wanakimbia vurugu zinazo endelea Nchini mwao ambapo kwa Mwezi january waliingia waomba hifadhi 2230, ambapo ilibainika wengi wao wanadai wanakimbia kukamatwa kwa kujihusisha na uhalifu na wengine kukimbia njaa iliyopo majumbani kwao.
Gaguti alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji wanaoingia Nchini wakidai kukimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha Vijana wa chama tawala kinacho julikana kama ( IMBONELAKULE), ambapo wanakuja kuomba hifadhi katika Nchi ya Tanzania ilihali Nchi yao ina amani ya kutosha na wengine kukimbilia kambini kupata huduma za bure kwa kuhofia njaa nchini mwao .
Hali iliyopelekea Waziri wa Mambo ya ndani kusitisha zoezi la Waomba hifadhi kuingia Nchini kwa kigezo cha kukimbia njaa Nchini mwao na kukimbilia Tanzania ili waweze kupata Msaada wa chakula , ni lazima Afanyiwe mahojiano na atoe sababu zilizo mfanya akimbie iliaweze kupatiwa kibali cha kuwa mkimbizi.
Hata hivyo Kanali Gaguti aliwaomba viongozi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini wahalifu hao waweze kurudishwa Nchini mwao kuepukana na vitendo vinavyo endelea na ongezeko la waomba hifadhi kuingia Nchini bila kufuata utaratibu.
'' leo nilikuwa natembelea vituo na kuona ongezeko la wahamiaji lakini serikali imetoa maelekezo mapya ikiwemo kuwatambua na kujua sababu za kukimbia Nchini mwao, lakini kama atakuwa na sababu za Msingi hata pata fursa ya kuwa mkimbizi, lakini pia nikuombe ushirikiano kama kuna taarifa za watu ambao ni wahalifu upewe taarifa mapema kabla ya mambo kubadilika ili tuweze kuchukua tahadhari mapema kwa pande zote mbili" alisema kanali Gaguti.
MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia, pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Burundi katika kujadiliana sakata la Wahamiaji wengi wengi kuanza kuingia nchini Tanzania kwa kasi tangu Januari,2017.
MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia
Mkuu wa Wilaya Ya Buhigwe akisalimiana Na Wanajeshi wa Burundi mpakani mwa Tanzania na Burundi
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama kuingia mpakani mwa Burundi na Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...