Waziri wa mambo ya katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe ametembelea Divisheni Maalum ya Mahakama inayojishughulisha na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi nchini Kanda ya Dar es Salaam na kujionea namna inavyoendesha shughuli zake.
Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Dkt Mwakyembe amewataka watendaji wa mahakama hiyo kuzingatia lengo la uanzishwaji wa mahakama hiyo ili kuleta tija na ufanisi uliofanywa kuanzishwa kwake.
“Mahakama hii ni chombo maalum kilichoundwa ili kushughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi ndani ya muda mfupi. Nyinyi kama watendaji hamna budi kuongeza bidii na kuhakikisha mashauri yote yanayoletwa katika mahakama hii yanamalizika ndani ya muda mfupi huku mkizingatia haki za kila mmoja na hivyo kufanikisha lengo la kuanzishwa kwake ”,alisema Dkt Mwakyembe
Aidha alisema uanzishwaji wa mahakama hiyo ulilenga kuifanya Tanzania kupunguza utendaji wa makosa ya aina hiyo au kuyamaliza kabisa na kuongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa inaonekana kuwa uhalifu wa aina hiyo umepungua.
Kutokana na kupungua kwa makosa hayo mhe. Waziri alisema anafikiria kuandaa mpango wa kupunguza kiwango cha gharama za makosa ambayo yatapelekwa mbele ya mahakama hiyo . “Inaonekana yale makosa ya ufisadi mkubwa hakuna kwa sasa na hili no moja ya lengo la kunazisha mahakama hii na kwa hali hiyo nafikiria kuja na mpango wa kupunguza kiwango cha thamani ya makosa ambayo kitakuwa ni chini ya kile kilichowekwa awali cha sh. Bilioni moja,” alisema Dr. Mwakyembe.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi uchumi alipoitembelea leo
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi uchumi alipoitembelea leo
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza kaimu mkuu wa mahakama hiyo Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Jaji Winnie Koroso alipokuwa akiatoa taarifa ya utendaji wa mahakama hiyo alipoitembelea leo
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza baada ya kufanya ziara katika Mahakama malum ya makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kanda ya Dar es Salaam leo
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia kitabu ambacho huingizwa orodha ya mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama maalum ya makosa ya rushwa na ufisadi alipoitembelea leo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...